KUITWA KWENYE USAILI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba Wizara, Idara zinazojitegemea na Wakala za Serikali (MDAs) anatarajia kuendesha usaili na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi, waombaji kazi watakaofaulu usaili.
Wasailiwa walioitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia yafuatayo:
1. Ukaguzi wa vyeti utafanyika saa 1:00 kabla ya muda wa mtihani wa mchujo kuanza.
2.Usaili utaanza saa moja na nusu asubuhi (1:30) na utafanyika mahali na tarehe kama inavyoonesha katika nafasi husika.
3. Kuja na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi mfano: kitambulisho cha mkazi, kupigia kura, kazi, hati ya kusafirian.k
4. Kuja na Vyeti Halisi (original certificates) vya kuanzia kidato cha nne, sita, Stashahada,Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za mwombaji.
5. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hatimatokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
6. Kila msailiwa aje na picha moja (Passport size).
7.Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
8.Kila msailiwa azingatie tarehe na eneo alilopangiwa kufanyiwa usaili
9.Kila msailiwa aje na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate)
10.Kwa wale waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU & NECTA)
11.Wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa maombi yao hayakufanikiwa na wasisite kuomba tena mara nafasi za kazi zitakapotangazwa.
******DOWNLOAD THE ATTACHMENT BELOW***** TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI
usipitwe.....<<<