logo blog

JOBS IN TANZANIA: KUITWA KWENYE USAILI - TBS - 06 Jan 2015

Shirika la Viwango Tanzania linapenda kuwatangazia waombaji wa nafasi za kazi katika kada za Standards Officer II na Records Management Assistant I, waliofanya usaili wa kuandika tarehe 06.01.2015 kuwa wafuatao wamechaguliwa kufanya usaili wa mahojiano utakaofanyika tarehe 08-01-2015 katika chumba cha mikutano TBS Ubungo saa mbili kamili asubuhi.
 
WASAILIWA WALIOITWA KWENYE USAILI WANATAKIWA KUZINGATIA YAFUATAYO.
i. Kuja na vyeti halisi (Original Certificates)vya kuanzia kidato cha nne,sita,stashahada,shahada ya juu,shahada,na kuendelea kutegemea na sifa za muombaji
ii. “Provisional Reslults” ,“Statement of Results” hati za matokeo za kidato cha nne na sita(form four and six results slips) havitakubaliwa
iii. Kuja na kitambulisho cha utambuzi mfano,hati ya kusafiria,kitambulisho cha mkazi,kupigia kura ,leseni ya udereva au kitambulisho cha kazi
iv. Kila msailiwa atajigharamia chakula,usafiri na malazi
v. Kila msailiwa azingatie tarehe na mahali pa kufanyia usaili
vi. Wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakufanikiwa.
Limetolewa na:
Kaimu Mkurugenzi Mkuu,
Shirika la Viwango Tanzania,
S.L.P 9524,
Dar es Salaam.

Tafadhali bonyeza linki ifuatayo ili uweze kuona orodha ya walioitwa kwenye usaili: