logo blog

MSAIDIZI WA OFISI (OFFICE ASSISTANT) (NAFASI 8)

MSAIDIZI WA OFISI (OFFICE ASSISTANT) (NAFASI 8) 
MAJUKUMU YA KAZI.
Kufanya usafi wa Ofisi na Mazingira ya nje na ndani ikiwa ni pamoja na kufagia,kufuta vumbi, kupiga deki, kukata majani, kupalilia bustani, kumwagilia maji bustani, kupanda maua au miti na kusafisha vyoo. .
Kuchukua na kupeleka majalada na hati nyingine kwa maofisa wanaohusika na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
Kusambaza barua za ofisi kama jinsi atakavyoelekezwa. Kutayarisha chai ya Ofisi.
Kupeleka mfuko wa posta na kuchukua barua kutoka Posta.
Kuhakikisha kwamba vifaa vya ofisi vinawekwa sehemu zinazostahili.
Kufungua Milango na Madirisha ya Ofisi wakati wa Asubuhi, na
Jioni kuyafunga baada ya saa za kazi.
Kurudufu barua au machapisho kwenye mashine za kurudufia.
Kuweka katika majalada nakala za barua zilizochapwa katika
ofisi walizomo.
Kutunza vifaa vya Ofisi na kutoa ripoti kila vinapoharibika.

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliofaulu vizuri katika
masomo ya Kiingereza, Kiswahili na Hisabati.
 
MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mishahara TGOS A kwa mwezi.

MASHART YA JUMLA KWA KAZI ZOTE:
1.    Waoombaji weote wawe raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45.
2.    Waombaji ambao tayari ni watumishi wa umma na wamejipatia sifa katika kada tofauti walizo nazo wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na waajiri wajiridhishe ipasavyo.
3.    Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha; kuto kuzingatia hili kutasababisha maombi kuwa batili.
4.    Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitoshereza (detailed CV) yenye anuani na namba za simu zaza kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
5.    Maombi yaambatane na nakala za vyeti vya taaluma, maelezo ,vyeti vya kidato cha nne au cha sita kwa wale waliofika kiwango hicho, vyeti vya kuzaliwa na vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wadondoka au kupotea. Astashahada/ stashahada/cheti, cheti za mitihani ya kidato cha IV NA VI, cheti cha kompyuta, picha moja ya “passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
6.     Testimonials “provisional result” statement of result hati ya matokeo ya kidato cha nne na sita (FORM IV AND VI RESULTS SLIPS) havitakubaliwa.
7.    Waombaji waombaji waliostaafishwa katika utumishi wa umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibari cha katibu mkuu kiongozi.
8.    Uwasilihaji wa taalifa na sifa za kugushi wahsika watachukuliwa hatua za kisheria.
9.     Mwiisho wa kupokea  barua za maombi ni tarehe 16 desemba 2014.
Maombi yanaweza kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili au kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo:- Mkurugenzi Mtendaji, 
Halmashauri ya Wilaya, Au
S.L.P.52,
Mkuu-Rombo.
District Executive Director,
Rombo District Council,
P.O. Box 52,
Mkuu-Rombo