JAMHURI YA MUUNGANO TANZANIA
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
TANGAZO
Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anapenda kuwatangazia Wauuguzi wa ngazi ya Astashahada na ngazi ya Stashahada waliohitimu mafunzo mwaka 2013wawasilishe maombi ya kupangiwa vituo vya kazi. Waombaji wanatakiwa kupendekeza maeneo matatu wanayotaka wapangiwe kazi.
Maeneo yenye nafasi za kazi yameainishwa kwenye tangazo la kazi kwenye tovuti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (www.moh.go.tz).
Maombi wayawasilishwe kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa anuani ya hapa chini kabla ya tarehe 14 Machi, 2014.
Katibu Mkuu,
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
S.L.P. 9083,
DAR ES SALAAM.
S.L.P. 9083,
DAR ES SALAAM.